30 Septemba 2015 - 15:31
 Polisi wavunja Kambi ya wahamiaji Italia

Polisi nchini Italia wameivunja kambi moja ya wahmiaji na wanaharakatio katika mpaka wa Italia na Ufaransa leo.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Polisi nchini Italia wameivunja kambi moja ya wahmiaji na wanaharakatio katika mpaka wa Italia na Ufaransa leo. Mwandishi mmoja wa Shirika la habari la Ufaransa AFP, amesema wahamiaji wamekimbilia mafichoni katika eneo moja la mlima karibu na sehemu hiyo kuepuka kukamatwa. Kambi hiyo mjini Ventimiglia ilikuwa  na karibu watu 50 na mji huo uligonga vichwa vya habari wakati  lilipoanza  janga la wahamiaji barani Ulaya mapema mwaka huu.  Msemaji wa polisi amesema kambi  hiyo imevunjwa kwa sababu wahamiaji  waliokuwa wakiishi mahala hapo wakitumia umeme na maji bila ya kulipia.

Mwisho wa habari/ 291